Cc Soseji za Farmers choice
Muda Kamilifu: Dakika 25
Kuandalia: 4
Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa ricipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, mlo wenye ladha tena wa kusisimua. Huku pwani kwetu ni cha mchana. Pepeta jiko tayari kutayarisha Pasta na mchuzi wa Soseji. Kampuni ya Farmers choice imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nitilie.
Viungo
Pakiti mbili za pasta unazopendelea, Mafuta ya Kupikia (3 tbspn), Soseji za Farmers choice-Spicy Beef Sausages Value Pack 1kg ( Pakiti 1) ,Pilipili hoho (2) (Rangi Nyekundu na manjano ), Kitunguu (1 iliyokatwa katwa kweenye vigae vidogo), kitunguu saumu 3 vilivyosagwa, Pilipili mbaazi (1tspn) ,Nyanya (6 kubwa zilizokatwa) ,Muchuzi wa Kuku (Kikombe ½) , Jibini (Kikombe ½ iliyokatwa) na chumvi Kiasi
- Katika sufuria kubwa, chemsha maji yenye chumvi kiasi kisha tia ndani zile tambi au pasta zako na uwache zichemke mpaka ziwe laini.
- Bakisha kikombe kimoja cha yale maji yaliyobakia kisha umwage hayo mengine. Tia tambi zako kando
- Eleka kikaangio tofauti kwenye jiko lenye joto la wastani kisha mimina mafuta yako. Yakipata joto, tia soseji zako pamoja na zile vitunguu. Kaanga kisha ongeza pilipili mbaazi na chumvi kiasi.
- Soseji zikianza kubadilisha rangi kuwa kahawia, ongeza kitunguu saumu na pilipili mbaazi kisha koroga kwa muda wa dakika 2 ivi.
- Ongeza ile nyanya, kisha koroga mpaka ule mchuzi uchanganike na soseji kabisa. Pika kwa dakika 3 ivi kisha mimina ule muchuzi wa Kuku ndani. Ongeza joto na kuiwacha iive mpaka itokote. Ongeza ile jabini kisha pika Zaidi kwa muda wa dakika 5 ivi mpaka mchuzi uwe mzito.
- Mtuzi wako ukiwa sawia, ongeza zile tambi (pasta) kisha koroga. Ongeza kile kikombe cha yale maji yaliyosalia na kuiwacha itokote kwa muda wa dakika 2-3 ivi.
- Epua na kuandaa mlo wako bila kungoja. Furahia!