Nyama Kavu

NYAMA KAVU
Cc Mafuta ya Rina
Total Time: 30 minutes
Serving:2

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa ricipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi.. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, mlo wa kusisimua. Huku pwani kwetu ni kiamsha. Pepeta jiko tayari kutayarisha Nyama Kavu. Mafuta ya Rina yamewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nitilie

Viungo

Nyama nusu ya ngombe, maziwa mala (5tbspn), kitunguu thomu kilichosagwa na tangawizi 2tbspns, pilipili mbuzi /paprika (2tbspn), mutton masala (1tbspn), pilipili manga (1tbspn), ndimu/limau Kiasi, Mafuta ya Kupikia ya Rina 2tbspn), chumvi Kiasi

 


MAELEZO YA KUPIKIA
Osha nyama uikate vipande Kiasi chako.
Weka mahitaji yote uchanganye vizuri kisha iache Kwa takriban dakika 30 au zaidi.
Weka ndani ya sufuria kisha ueleke kwenye jiko lako la makaa / au gesi na uhakikishe moto ni mdogo mdogo ili nyama iive pole pole. (30-40 dakika)
Nyama yako iko tayari. Andaa mezani Kwa chips, mkate wa mofa au hata wali.

MAZINGATIO
1. Andaa nyama ikiwa Moto Moto la sivyo itaganda na pia Itakuwa ngumu.
2. Ni vizuri nyama hii iwe kavu au ubakishe supu kidogo sana ili viungo viingie kwenye nyama vizuri.
3. Usiweke maji hata kidogo kama hupiki na pressure cooker.Nyama itatoa maji yake yenyewe ambayo yanatosha kuiivisha.

You are currently viewing Nyama Kavu

Leave a Reply