Mishikaki ya Kuku

Muda Kamilifu:  Dakika 35

Kuandalia: 8

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa ricipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, mlo wenye ladha tena wa kusisimua. Huku pwani kwetu ni cha jio. Pepeta jiko tayari kutayarisha Mishikaki ya Kuku. Kampuni ya Quality Meat Packers , QMP choice imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nilishe.

Viungo

Kilo 1 ya Kuku isiyo Mifupa (Kata kata kwa Vigae wastani- inchi 1 au  1-1/2 ), 1 Tsp ya Mafuta ya olive , 2 Tbsp ya Pilipili manga, Chumvi (Kiwango kinachokufaa), 1/4 Tsp ya paprika tamu, 1 Tbsp ya Bizari nyembamba, 1 Tbsp ya garam masala, 1/4 Tsp ya Kitungu saumu (Unga) , 1/4 ya Tsp thyme iliyokaushwa, Miti 6 ya Kuchoma Mishikaki , 30 ml-maji ya Limau , Pili Pili hoho- 1 kubwa ya kijani (Kwa hiari yako), Pili pii hoho – 1 kubwa ya manjano (Kwa hiari yako)

Maelekezo

Changanya ile nyama yako ya kuku na zile viungo vyako

Nyunyuzia 30 ml ya yale maji ya kimau kisho nyuyuzia kijiko kimoja ya mafuta ya olive kasha endelea kuchanganya mpaka vichanganyike vizuri

Wacha ile nyama ikae kwa muda wa lisaa limoja ili ikolee viungo yaani imarinate vizuri

Baada ya hilo lisaa, panga nyama yako kwa vile vijiti vya kuchoma ukitia pipipili hoho katikati ya vile vigae vya nyama mpaka mishikaki yote yaishe.

*Hakikisha Loa zile mishikaki kwa maji kwa dakika 10 ivi kabla ya kuvitumia ili kuepuka visichomeke*

Pakiza mafuta kwenye Kikaangio chako kisha kuchoma zile mishikaki pande zote mbili mpaka ziive. Dakika 25 ivi kila upande.

Lea ile mishikaki kwa sosi ya ukwaju na wali mweupe.

Chakula chako kipo jikoni tayari kwa kuwashangaza wale wote walioudhuria kwa kula chakula chenye ladha safi. Enjoii.

 

You are currently viewing Mishikaki ya Kuku

Leave a Reply