MCHUZI WA VIAZI VITAMU NA MCHUZI WA KARANGA

 

Cc nutgoldke

TOTAL TIME: 1 hr 5 mins

Serving: 6

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa ricipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi.. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, mlo wa kusisimua. Huku pwani kwetu ni Chakula cha Mchana au cha jio. Pepeta jiko tayari kutayarisha Mchuzi wa Viazi Vitamu na Mchuzi wa Karanga. NutGold Peanut Butter imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nitilie.

INGREDIENTS

Vijiko 1 ½ vya Mafuta ya Mboga,  Kitunguu 1 Kubwa – Kata kata kwa vigae vidogo, Vitunguu saumu-2 (iliyokunwa), 1 ginger inchi tangawizi safi, iliyosafishwa na iliyokunwa (vijiko 1½), Kijiko ¼ ya chumvi, Kijiko ½ tsp pilipili nyeusi, Kijiko 1 pilipili ya cayenne, Kijiko 1 tbsp dhania, Vijiko 2 vya pilipili Nyekundu – iliyokatwa vizuri, 150 g ya Nut gold smooth peanut butter, 400 g ya Nyaya ikiyo katwakatwa na (2) viazi vitamu – iliyokatwakatwa kwa vigae vinavyofaa

MAELEZO YA KUPIKIA

  1. Pasha joto yale mafuta ya mboga kwenye kikaangio
  2. Ongeza zike vitunguu kicha upike kwa muda wa dakika tano kwenye moto wastani mpaka ziwe nyororo
  3. Baada ya dakika tano ivi, ongeza tangawizi, Kitunguu sumu, chumvi, pilipili, dhania kisha koroga na upike Zaidi kwa dakika 2-3 ivi
  4. Ongeza joto ya upishi, kisha utie karanga yako ya Nut Gold, nyanya, na viazi tamu. Pika mpaka ichemke kisha punguza joto na ufunike kikaangio chako. Chemsha kwa dakika 30, ukichochea muda kwa muda.
  5. Baada ya dakika 30, toa ile kifuniko, ongeza karanga kiasi na dhania kisha pika kwa dakika zingine 2 ili mchuzi upate uzito unaofaa
  6. Zima jiko lako na uepue chakula chako kwa mchele na sukuma wiki.

 

 

 

You are currently viewing MCHUZI WA VIAZI VITAMU NA MCHUZI WA KARANGA
MCHUZI WA VIAZI VITAMU

Leave a Reply