MCHUZI WA SAMAKI WA MACKEREL WA NAZI

MCHUZI WA SAMAKI WA MACKEREL WA NAZI
Cc Kara Coconut Milk
Total Time: 1 hr
Serving: 6

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa ricipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi.. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, mlo wa kusisimua. Huku pwani kwetu ni Chakula cha Mchana au cha jio. Pepeta jiko tayari kutayarisha Mchuzi wa Samaki wa Mackerel wa Nazi. Kara Coconut Milk imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nitilie

mackerel-with-fresh-peppercorn-and-coconut-milk-6

Epua kwa Wali mweupe ama viazi zilizosokotwa na utakuwa na mlo wa kufaana kupindukia ama wasemavyo wamerika a Match made in Heaven
Viungo
4 mackerels, 2 Vikombe vya Tui ya nazi ya Kara , Kijiko 1 cha pilipili Nyekundu , Majani ya curry kama 10 ivi, 1 – Kitunguu Kubwa iliyo katakatwa kwa vigae vidogo , 2 au 3 – Pilipili Kali ya Kijani , Kijiko 1 poda ya manjano( turmeric powder), Kijiko 1- poda ya coriander , Chumvi, Mafuta ya kupikia , Limau 1 ( Iliyokatwa)

MAELEZO YA KUPIKIA

Kwenye Kikaangio chako, kaanga yale majani ya curry kwenye kijiko kimoja cha mafuta kwa muda wa dakika 2 ivi kisha nyunyuzia maji ya limau kisha chumvi. Ikiiva weka kando kwenye chombo

Osha kisha katakata ule samaki wa Mackerel kwa vigae 3 kila moja. Ongeza vile vigae katika kile chombo

mackerel-with-fresh-peppercorn-and-coconut-milk-5

Katika kile chombo ongeza poda ya manjano na pilipili Nyekundu kisha wacha itulie kwa muda was aa moja ivi.

Kaaga Samaki wako kwenye mafuta yenye joto kwa dakika 5 ivi kila upande kisha uweke kanado

Soma zaidi Cuisines You Should Never Miss While In Coast Of Kenya
Kwenye kikaangio kingine, pasha joto mafuta vijiko 2 kisha ongeza vitunguu. Ongeza chumvi kisha pika vitunguu vyako hadi view nyororo. Kisha, ngeza poda ya coriander kisha pika kwa dakiki zingine 2.

mackerel-with-fresh-peppercorn

Ongeza pilipili kisha zile Majani za curry na ukoroge. Chukua tui yako ya nazi ya Kara na uongeze kwenye ule mchuzi Pamoja na chumvi kiasi kisha wacha iive kwa dakika kidogo. Hatimaye, ongeza samazi wako uliokaangwa na upike kwa dakika 2 ivi.
Epua chakula chako kwa mchele ama viazi zilizosokotwa

You are currently viewing MCHUZI WA SAMAKI WA MACKEREL WA NAZI
mackerel-with-fresh-peppercorn

Leave a Reply