Mapishi ya kababu za Nyama ya Kusaga

Cc Mafuta Ya Avena
Muda Kamilifu: Dakika 40
Kuandalia: 5

Avena Vegetable Cooking Oil 5L

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa recipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, chakula chenye ladha mno. Pwani, mlo huu una umaarufu sana. Kama hujawahi kukitumia, basi baada ya kusoma makala hii utakua mdau muhimu wa kitafunio hichi. Pepeta jiko tayari kutayarisha kababu za Nyama ya kusaga. Kampuni ya Golden Africa Kenya Ltd kupitia mafuta ya kupikia ya Avena, imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nilishe.

Hisani KA=ababu za nyama

Viungo
Nyama ya kusaga Kilo 1, Kitunguu maji kikubwa 1, Vitunguu thomu punje kubwa 3, Tangawizi kijiko Cha Chai1(ilotwanga), Pilipili ya kuwasha 1(au zaidi kama mpenzi wa pilipili), Ndimu 2, Pilipili manga ya unga nusu kijiko cha chakula, Mdalasini wa unga nusu kijiko cha chakula, Uzile(Binzari nyembamba) ya unga Kijiko Cha Chakula 1 (Cumin powder), Mafuta ya kupikia ya Avena nusu lita, Karoti ndogo 1(ilioparwa), Bizari ya Kababu au Kebab Masala ½ paketi, Chumvi kiasi, Mayai 3 na Bread crumbs kikombe kidogo kimoja

Mapishi ya kababu za nyama

Maelekezo
1.Weka nyama Yako katika bakuli kubwa kisha gawa nyama yako sehemu mbili sawa
2. Moja weka jikoni tia chumvi,ndimu usiweke maji acha itoe maji yenyewe hadi iwive Kisha changanya nyama mbichi na iloiva pamoja
3. Twanga kitunguu thomu,pilipili na chumvi na uviweke kwenye nyama
4. Changanya nyama yako vizuri weka tangawizi,pilipili manga,mdalasini,uzile na uichanganye vizuri
5. Menya kitunguu maji, vikate kate na viweka kwenye nyama
6. Weka Kebab masala kama unayo na uchanganye mchanganyiko wako Weka Kebab masala kama unayo na uchanganye mchanganyiko wako
7. Malizia kuweka Bread crumbs zako changanya mchanganyiko wako na onja chumvi kama haijakolea ongeza kidogo na uchanganye vizuri mchanganyiko wako
8. Chukua nyama yako fanya madonge shape ya maduara madogo madogo mpaka umalize nyama yako.
9. Andaa kibakuli kingine vunja mayai yako yalobakia weka na chumvi kidogo yachanganye na kijiko au umma na yaweke pembeni
10. Weka mafuta yako ya Avena kwenye karai yaache yapate moto sana kisha chukua maduara yako yachovye kwenye mayai kisha dumbukiza kwenye mafuta
11. Kaanga kwa dakika 3 kisha zigeuze na ziwache kidogo kama sambusa mpaka Zibadilike rangi.
12. Zikiwa za brown zitoe weka kwenye chujio au tissue zichuje mafuta
13. Unaweza kula kababu zako na Chapati au mkate wowote ule. Inapendeza uweke na chatne wakati wa kula

 

Angalizo
1.Ili kababu zipendeze hakikisha zinachapuka viungo vizuri
2. Hakikisha Mafuta yamepata moto vizuri, yasipopata moto vizuri kababu zinaweza kupasuka kwenye mafuta

3. Mayai ya kuchovyea wakati wa kupikia yawe ya kutosha

 

You are currently viewing Mapishi ya kababu za Nyama ya Kusaga
kababu za nyama

Leave a Reply