Muda Kamilifu: Dakika 40
Kuandalia: 8
Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa recipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, chakula chenye ladha mno.

Pwani, mlo huu una umaarufu sana. Kama hujawahi kukitumia, basi baada ya kusoma makala hii utakua mdau muhimu wa kitafunio hichi. Pepeta jiko tayari kutayarisha kababu za Mboga. Kampuni ya Golden Africa Kenya Ltd kupitia mafuta ya kupikia ya Avena, imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nilishe.
Viungo na Vipimo:
Viazi 2 (vichwadondoa na kukata kete), Karoti 1 (vichwadondoa na kukata vipande), Maharage ya kijani (chop) 5, Maharage ya njano (chop) 5, Mahindi matamu 3 tbsp, Maharage ya kunde 2 tbsp, Kabichi 6, Chumvi ½ tsp, Unga wa mahindi robo kikombe, Unga wa pilipili manga ¾ tsp, Garam masala ½ tsp, Unga wa bizari ¼ tsp, Unga wa embe kavu ½ tsp, Tangawizi na vitunguu maji ½ tsp, Mint 2 tbsp (ilokatwakatwa vizuri), Dhania 2 tbsp (ilokatwakatwa vizuri), Breadcrumbs 2 tbsp na Mafuta ya kukaangia y Avena
Maelekezo
1.Chukua mboga zilizopikwa na uzikande vizuri katika bakuli kubwa la kuchanganyia.
2. Ongeza unga wa mahindi robo kikombe.
3. Kisha, ongeza viungo vyote, tangawizi na vitunguu maji, mint, dhania, na chumvi.
4. Changanya vizuri kuhakikisha kuwa viungo vyote vimechanganyika vizuri.
5. Ongeza breadcrumbs na changanya vizuri.
6. Chukua kijiti cha barafu na uzungushe mchanganyiko huo.
7. Kaanga kebab kwenye tawa yenye mafuta ya Avena yenye moto.
8. Paka mafuta na kaanga kwa moto wa wastani kwa dakika 3 kisha zigeuze na ziwache kidogo kama sambusa mpaka Zibadilike rangi.
9. Zikiwa tayari zitoe kisha weka kwenye chujio au tissue zichuje mafuta
10. Unaweza kula kababu zako na Chapati au mkate wowote ule. Inapendeza uweke na chatne masala na chatne ya kijani wakati wa kula

Angalizo
1.Ili kababu zipendeze hakikisha zinachapuka viungo vizuri
2. Hakikisha Mafuta yamepata moto vizuri, yasipopata moto vizuri kababu zinaweza kupasuka kwenye mafuta

3. Mayai ya kuchovyea wakati wa kupikia yawe ya kutosha