Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa ricipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Si mapochopocho, si mlo mku…usibanduke katu, rai kaa kitako tutie ndani pamoja. Usiogope kusisitiza mama nitilie. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, mlo wa kusisimua. Huku pwani kwetu, ni chamsha kinywa ama cha mchana. Pepeta jiko tayari kutayarisha Kababu za mayai au ukipenda Meatballs stuffed with Egg. MAISHA FLOUR imewezesha mapishi haya
Vipimo
Nyama ya Kusaga – Kilo 2 ,Mayai yaliyochemshwa-8, Tangawizi na Kitunguu saumu iliyosagwa – Kijiko 1 , Pilipili mbichi ya kusaga- 2, Mafuta- Vijiko 2 vya supu, Unga ya MAISHA- Kijiko 2 ,Kitungu- 1 kubwa iliyokatwa, Chumvi – Kipimo ya kujifaa, Bizari ya manjano , Dania ya unga, Bizari ya Pilau ( zote ¼ kijiko cha chai )
Maelekezo
-
Changanya nyama, kitungu, dania, tandawizi, kitunguu saumu, na unga ya MAISHA kisha tengeneza mahari.
-
Kisha gawanya madonge 8 yaliyosawa
-
Chukua donge moja kisha tia ndani yake yai uliochemsha na lifunike vizuri
-
Ukisha maliza kuyafunika yote, yapange kwenye treya la kupikia katika jiko la oveni, nyunyuzia mafuta kidogo na choma moto wa 275F kwa muda wa sakika 25
-
Yakishaiva epua na kisha ukate kwa vigae viwili tayari kuliwa
Andaa mlo wako tayari kudishy na mchuzi wa nyaya na sharubati – tosha jienjoi.