MAMA NITILIE
Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, mlo wa kusisimua. Huku pwani kwetu, Kifungua kinywa sio kifungua kinywa bila mlo huu. Pepeta jiko tayari kutayarisha Mahamri na mbahazi za nazi. Tui ya KARA imewezesha mapishi haya
Viungo
Mbahazi zilizo chemshwa
Tui zito
Tui nyembamba
Kitungu saumu ilo pondwa
Bizari
Pilipili boga
Jinsi ya kutayarisha
- Kwenye sufuria,weka mbahazi zako zi chemke na tui nyembamba (coconut milk)
- Weka saumu na bizari na chunvi kidogo ya kuongeza ladha
- Wacha itokote kwa mda wa dakika kumi tui lipungue
- Weka tui zito juu kisha koroga kwa utaratibu
- Subiri ipoe alafu mimina tui zito(coconut cream)juu
- Pamba mbahazi zako na pilipili boga na dhania juu kwa harufu na ladha bomba zaidi
- Burudika na mahamri na chai
Pingback: Cuisines You Should Never Miss While In Coast Of Kenya - DISHY KENYA