Cc Salit
Muda Kamilifu: Dakika 30
Kuandalia: 5
Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa ecipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, Kitafunio chenye ladha mno. Pwani, kitafunio hiki kina umaarufu sana. Kama hujawahi kukitumia, basi baada ya kusoma makala hii utakua mdau muhimu wa chakula hichi. Pepeta jiko tayari kutayarisha Kachiri ya Muhogo . Kampuni ya Kapa oil kupitia mafuta ya kupikia ya Rina, imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nilishe.
Viungo
Kilo 1 ya Muhogo, 1/2 litre ya Mafuta ya kupikia ya Salit, 2 Tsp ya pilipili unga, 30 ml-maji ya Limau, Chumvi (Kiwango kinachokufaa)
Maelekezo
1.Chagua Mihogo yako ukizingatia ziwe nyororo kwa ladha ya kufaanya zaidi na pia urahisi wa kuikata kata kisha osha mpaka ziwe safi.
- Menya zile Mihogo kisha zikate kate kwa vigae vyembamba kama vile crisps ama utumie machine ya kukukata ili kupata uembamba unaofaa
- Baada ya kuvikakatakata vyote, weka vile vipande kando.
- Kwa Kikaangio kikubwa eleka ile mafuta yako ya salit na kuipasha moto mpaka iwe moto.
- Tumbukiza zile mihogo iliyokatwakatwa pole pole na kukoroga kwa upole ukihakikisha zile vipande havijashikana.
- Pika mpaka ukingo wa vile vipande vigeuke rangi ya hudhurungi kisha hamisha kwa bakuli tofauti
- Nyunyuzia ile pilipili yako, chumvi na maji ya limau kisha changanya pole pole kwa zile kachiri.
Kachiri zako ziko tayari. Enjoi