Jinsi ya Kutayarisha Kuku ya Mandi

 

Cc Rina Cooking Oil

Muda Kamilifu:  Dakika 50

Kuandalia: 5

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa Recipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, Chagio chenye ladha mno. Pwani, mlo huu una umaarufu sana. Kama hujawahi kukitumia, basi baada ya kusoma makala hii utakua mdau muhimu wa chakula hichi. Pepeta jiko tayari kutayarisha Mandi ya Kuku. Kampuni ya Kapa oil kupitia mafuta ya kupikia ya Rina, imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nilishe.

 

Viungo vya Kuku

Vipande 2 vya mapaja ya kuku, 1 kitunguu maji ( katakata), 5 tbsp mafuta ya Kupikia ya Rina and matunda makavu ya Lozi (Almond)

Viungo vya Kukolea

1 tbsp mbegu za bizari ,1 tbsp curry powder, 2 chembe za mdalasini , ½ Tsp pilipili manga, 1 tangawizi, 3 chembe za iliki, 1 tbsp kitunguu saumu, Chumvi (inavyokufaa)

 

Viungo vya Mchelle

Vikombe 2 mchele wa Basmati uliooshawa na kuroweka , 30ml kidonge cha supu ya kuku (chicken broth)

 

 

Maelekezo

 

1.Kwenye Kikaangio chenye moto mdogo kanga zilie chembe za lozi kwa dakiki 2-3 kisha ziweke pembeni

 1. Katika kile kikaangio chako, weka bizari, mbegu za bizari na chembe za mdalasini kisha wacha zipashe moto kwa dakika 2-3. Ongeza viungo vingine vya unga -curry powder na pilipili manga kisha zikaange kwa muda wa dakika 2 na uviweke pembeni kwa dakika 3.
 2. Zisage kwenye blender mpaka ziwe unga laini
 3. Zigawe viungo zako mara mbili. Moja iweke pembeni na ya pili ichanganye na mafuta kijiko 1 ya Rina mpaka itengeneze mchanganyiko laini na mzito kiasi. Tia chumvi kiasi
 4. Pakaza ule mchanganyiko kwenye kuku wako mpaka ienee vizuri. Funika na kuwacha ikolee viungo kwa dakika 30.
 5. Kwenye kikaangio tofauti, weka mafuta ya kupikia ya Rina vijiko 3. Ongeza vitunguu na Kuvikaanga kwa dadika 2-3. (Hakikisha zisiive sana au kupata rangi ya hudhurungi).
 6. Weka vipande vyako vya kuku vilivyo kolea viungo na uvikaange kila upande dakika 2 kwa moto wa wastani. Hakikisha kuku hazigandi
 7. Ongeza maji ya wastani yanayoweza ivisha Kuku wako kisha zifunike mpaka ziive vizuri, ukigeuza kila mara. Kuku wako akiiva mtoe kwenye ile supu na kumueka pembeni

Soma zaidi Kababu Za Mayai

9.Hakikisha ile supu uliyoibakisha inaiva na unaweza kuongeza ili iwezi kuivisha mchele wako. Ongeza bizari, tangawizi, saumu pamoja na kidonge cha supu ya kuku kisha koroga.  Weka mchele ambo umeroweka na kisha funika hadi uchemke na kukauka.

 1. Chukua ile sehemu ya pili ya viungo uliyoweka pembeni na kuchanganya na mafuta yaliyobaki Ongeza pilipili hoho tsp 2 kisha ipakaze ile kuku uliyotia pembeni.
 2. Choma ile kuku kwa makaa ama kwa oven, kadri inayokufaa kwa muda wa dakika 20.
 3. Mchele ikiiva unaweza ongeza matunda yako ya lovi na kuwacha ilainike kwa dakika 10.
 4. Wali ukiiva, weka kuku wako ambao umemchoma kisha chukua kaa la moto uweke kwenye chombo (kikombe) na kutia mafuta ya kupikia kwenye kile chombo ( kwa lengo la kufukiza) kisha iweke kwenye ile mchele na kufunika hicho kikaangio kwa dakika 2-4 ivi.
 5. Epua.

 

 

 

You are currently viewing Jinsi ya Kutayarisha Kuku ya Mandi

This Post Has One Comment

Leave a Reply