Chapati Za Malenge

Chapati Za Malenge Laini Na Tamu Sana
Cc Unga wa chapati wa Taifa
Muda Kamilifu: Saa 1
Kuandalia: 10

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, MAMA NILISHE. Hapa nitakupa Recipe mingi na jinsi ya matayarisho yake, kwa njia rahisi tena ya kufaana. Katika toleo hili, kila kitu ni cha kawaida, kwa hivyo kitashangaza na kufurahi kwa urahisi. Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa, chakula chenye ladha mno. Pwani, mlo huu una umaarufu sana. Kama hujawahi kukitumia, basi baada ya kusoma makala hii utakua mdau muhimu wa kitafunio hichi. Pepeta jiko tayari kutayarisha Chapati za Malenge. Kampuni ya Mombasa Maize Millers kupitia Unga wa chapati wa Taifa, imewezesha mapishi haya. Usiogope kusisitiza mama nilishe.

Chapati za Malenge

Viungo vya Chapati

3 Vicombe- Taifa all-purpose flour,1 Kikombe- Maji fufutende ,Chumvi-1 Tsp ,Sukari-1 Tsp (Ukipenda),400g ya Malenge na 1/4 L -Mafuta ya kupikia oil

Maelekezo

1.Tayarisha ile malenge kwa kwanza kuikata katika vigae vya wastani kisha vichemshe kwa muda wa dakika 15 au hadi vilainike
2. Vikisha kuwa nyororo, chuja yale maji kisha visha panya ile malenge hadi iwe laini.
3. Kwenye bakuli tofauti weka maji (400 ml) yawe ya uvuguvugu kisha tia chumvi na koroga vizuri ichanganyike.
4. katika bakuli kubwa ya kukandia, tia ile malenge iliyopondwa pondwa, tia unga wa chapati wa Taifa, kisha tia mafuta kama vijiko vinne vikubwa katika unga.
5. Tia maji katika unga na anza kuukanda, kanda mpaka uone umechanganyika mpaka ushikane na ulainike vizuri kisha utengeneze donge moja kubwa.

Soma zaidi Yellow Tumeric Vegetable Rice
6. Funika unga kisha ueke pembeni Kwa takriban dakika 30(ukieka Kwa muda mrefu zaidi ndio utalainika zaidi)
7. Funua unga wako utoe madonge matatu(size ya madonge itategemea na mahali pako pa kusukuma. Kama ni pakubwa unaweza hata ukafanya donge moja Tu)
8. Sukuma donge moja moja kama chapati kisha upake mafuta na ukunje kama swissroll(kufanya tabaki)
9. Gawanya size unayotaka na ukunje vizuri chapati zako. Ziwache tena Kwa takriban nusu saa au zaidi ili zizidi kulainika
10. Bandika chuma cha kuchomea chapati motoni na uache kishike moto
11. Chuma kikiendelea kushika moto, sukuma chapati zako size unayotaka (zisiwe nene wala nyembamba Sana)
12. Chuma kikishashika moto, weka chapati uanze kuchoma
13. Chapati ikishika rangi  kidogo upande mmoja,geuza upande wa pili pia ishike rangi. Weka mafuta upande mmoja na uipike chapati Kwa sekunde kadhaa huku ukiemezea chini Kwa kitambara au kijiko kikubwa ili ikolee rangi nzuri.
14. Geuza upande wa pili ufanye vivyo hivyo.
15. Chapati zipo tayari

Chapati za malenge

Maelezo Ya Ziada
1.Ongeza unga wa maziwa takriban vijiko 3_4 vya mezani itasaidia chapati kuwa laini zaidi
2. Usiiwache chapati Kwa muda mrefu kwenye moto kwasababu itakuwa kavu
3. Usiwache wazi madonge yako ya chapati au unga baada ya kuukanda kwasababu unaweza ukafanya ukoko juu

You are currently viewing Chapati Za Malenge
Chapati za Malenge

Leave a Reply