Bazari ya Nazi

Bazari ya Nazi

Bazari ya Nazi ni mlo maarufu sana unaoliwa sana huku kwetu pwani kama chamsha kinywa. Mbaazi ya thelathini na mandazi au Mahamri 5 ivi ni chamsha kinywa tosha kabisa. Matayarisho yake nyumbani si ngumu kamwe, basi keti kitako nikuonyeshe jinsi ya kutengeneza chamsha kinywa ya kufaana. Ni mimi wenyu MWANAIDI SHISHI ukipenda niite MAMA NITILIE

Vinavyohitajika

 1. Kikombe 1 cha tui nyepesi na Kikombe ½ cha tui nzito
 2. Kijiko 1 cha Barazi , Iliyo chemshwa kisha kuloweshwa majini usiku nzima
 3. Kitunguu 1 kubwa, – ikate kate kwa vigae vidogo
 4. Iliki 2- Vikunwe
 5. Tangawizi 1 – Ikunwe
 6. Pilipili 3- Vitatwekatwe
 7. Kijiko ¼ ya Manjano ya unga
 8. Kikombe ½ ya Dhania (Giligilani)- Ikatwe saana
 9. Kijiko 1 cha Mafuta
 10. Chumvi kwa upendeleo wako

Jinsi/ Namna

 1. Eleka mafuta kwenye sufuria yako ya kupikia hadi mafuta yapate joto kiasi. Kaanga Kitunguu kwa mafuta hadi zigeuze rangi lakini zisiungue.
 2. Kisha ongeza Barazi , Iliyo chemshwa pamoja na ile tui.
 3. Ongeza iliki, tangawizi , pilipili, manjano halafu kisha chumvi.
 4. Funika na kuiwacha iive kwa muda wa dakila 30. Ikiwa nzito sana, ongeza maji kiasi. Ongezea dhania kwa mlo wako kisha iweke kando.
 5. Kwa sufuria tofauti, pasha moto tui ile kwa moto wa wastani. Inapo pata joto, koroga kwa maendelezo radhi isishike chini ya sufuria kwa muda wa dakika 10 hadi iwe nzito.
 6. Nyunyuzia au umwage ile tui juu ya ile Barazi au Mbaazi iliyoiva; Ifunike na kuiwacha itulie kwa muda wa dakika 15 kabla ya kukoroga na kupakua.

Pakua chakula chako kikiwa kungali moto tayari kutiwa ndani na mandazi kama kiambatanishi.

Next PostRead more articles

Leave a Reply