Samaki Wa Kupaka Tui La Nazi La Bizari Mchanganyiko

Vipimo

Samaki mkubwa – 1

Tui la nazi zito – 2 vikombe

Pilipili mbuzi -1

Pilipili mbichi kijani -2

Bizari mchanganyiko 2 Vijiko vya chai

Bizari ya manjano  ½  kijiko cha chai

Ndimu -1 kamua maji

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Msafishe samaki mweke achuje maji
  2. Katika kibakuli kidogo, weka Tui, pilipili mbichi, pilipili Mbuzi, Bizari na chumvi kisha tia mchanganyiko huo katika mashine ya kusagia (blender)
  3. Teka kidogo kisha mroweke samaki kwa mchanganyiko huo wa tui au umpake samaki kwa mchanganyiko ule kisha mwache samaki katika friji muda kiasi nusu saa au zaidi yake.
  4. Paka mafuta kidogo treya ya samaki, mweke samaki kisha mchome kwa moto wa juu katika oveni (Grill)
  5. Akiwiva upande mmoja mgeuze upande wa pili huku ukimpaka tui kisha mwepue na umweke katika sahani ya kupakulia.
  6. Katika sufuria ndogo, weka ule mchanganuiko wa tui ulio iweka kando, wacha ichemke kidogo tu huku ukikoroga kwa moto mdogo kiasi cha dakika moja .Rojo likianza kuwa zito tia ndimu.
  7. Epua na kisha mwagia juu ya samaki.  Tayari kuliwa.