Mama Nitilie Mkate wa Sinia

Karibuni wadau, usitiwe na kiwewe hataa kwani ushafika kwenye jukwaa la mapishi yangu, mama nitilie. Hapa nitakupa ricipe mingi na jinsi ya matayarisho yake , kwa njia rahisi tena ya kufaana. Si mapochopocho, si mlo mku…usibanduke katu, rai kaa kitako tutie ndani pamoja. Usiogope kusisitiza mama nitilie.

Leo tunapotandaza mkeka kwenye veranda tumo tayari kuandaa , mlo wa kusisimua. Huku pwani kwetu, ni kiteremsho haswaa masaa ya jioni na kahawa tamu ama asubuhi na chai ya iliki kama Kiamsha Kinywa. Pepeta jiko tayari kutayarisha Mkate wa sinia au ukipenda Mkate wa Kumimina

Mkate Wa Sinia / Mkate Wa Kumimina

Vipimo

 • 1 Kikombe cha mchele
 • 1 Kikombe cha Nazi ya Unga
 • 1 Kikombe cha sukari kupungua Kidogo
 • 1 Kikombe cha maji au maziwa vuguvugu
 • 1 Kijiko cha chai cha Hamira
 • Iliki kiasi upendavyo
 • Ute wa Yai moja

Namna Ya Kutayarisha Na Kuipika

 1. Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
 2. Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka  mchanganyiko uwe lani kabisa.
 3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
 4. Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
 5. Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
 6. Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
 7. Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata. Ni bora kuula siku ya pili yake.